8/14/2004

Rais wa Tanzania lazima...

Nitaanzisha kampeni ya kuweka kipengele kwenye katiba kinachosema kuwa Rais wa Tanzania lazima awe anafanya mazoezi ya mwili, si chini ya mara tatu kwa wiki. Pia lazima awe anakula chakula bora ambacho ni mboga kwa wingi, maji si chini ya bilauri nane kwa siku, na matunda. Vyakula hivi lazima viwe havina homoni au kemikali, na visitokane na mbegu za kijenetiki. Chakula cha Rais lazima kiwe kimetokana na jasho la wakulima wa Tanzania (yaani hakuna kula chakula toka nje ya nchi). Kwanini Rais wa nchi ambayo inadai kuwa kilimo ni uti wa mgongo ale matunda, maji ya mtunda, mboga, n.k. toka nje ya nchi?

Kutakuwa na kipengele pia kisemacho kuwa Rais akiwa na kitambi (yaani tumbo lililojaa mafuta yasiyotumika na wala kuhitajika mwilini) itabidi ajiuzulu! Naona itabidi pia kuwe na kipengele ambacho kinamzuia Rais kwenda kutibiwa nje ya nchi. Hii itamfanya ahakikishe kuwa nchi ina madaktari na vifaa vya matibabu vya kisasa kwa ajili yake na wananchi wake.

Kwanini tuwe na Rais ambaye hatunzi afya yake? Akishindwa kutunza mwili wake binafsi atawezaje kutunza nchi nzima????

Lakini msije mkasema kuwa haya ni madongo namtupia Rais Mkapa. Haya ni yenu mnayazua! Mimi humo simo.

1 Maoni Yako:

At 8/15/2004 04:51:00 AM, Blogger Maka Patrick Mwasomola said...

Ninafikiri unamaanisha Rais ajaye yaani Rais wa wakati ujao.Ni kweli maana kama Rais atakwenda nje kutibiwa wakati anapata vyakula vya kiasili vilivyotokana na wakulima wa humuhumu nchini itabidi hao madaktari wawajibike.Maana vitakuwa ni vyakula ambavyo havijatokana na jenetik wala kuwekwa au kuongezwa vitu vovyote ambavyo siyo vya kiasili.

 

Post a Comment

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com