3/09/2005

MAHESABU YA MWIZI WA TANZANIA OKTOBA MWAKA HUU

Rafiki yangu wa karibu ambaye ni mwana uchumi, baada ya kusoma makala yangu hii hapa iitwayo TUBINAFSISHE IKULU, ameamua kunipa mahesabu yatakayosaidia kupata rais au mwizi (kutegemea na mtazamo wako) kupitia moja ya mapendekezo niliyotoa kwenye makala hiyo. Huu hapa chini ndio ujumbe wake:
Baada ya kusoma makala yako ya kubinafsisha ikulu nimeona kwamba pendekezo ambalo litafanyika ni lakwanza; yaani kuwa na rais mwislamu na mkristo. Litafanya kazi kama hivi: Rais akiwa Mwislamu makamu wake ni Mkristo. Sasa mahesabu ni kama ifuatavyo:
1. Mwislamu+Mwislamu = haiwezekani
2. Mkristo +Mkristo = Haiwezekani
3. Mwislamu+ Mkristo= Inawezekana.

Sasa hesabu zitafanya kazi kama hivi:Kwa vile Kikatiba ni lazima Rais akitoka bara makamu atoke Zanzibar; Kama Rais atatoka Bara ni Lazima awe Mkristo kwa vile Zanzinbar hapatakuwa na Mkristo wakuwa makamu wa Rais. Kama Rais atatoka Zanzibar ambapo ni mwislamu basi makamu toka bara ni lazima awe Mkristo. Kwa mantiki hiyo basi kuna uwezekano kuwa mgombea yeyote kutokaBara atakuwa Mkristo ili mgombea mwenza toka Zanzibar awe mwislamu. Kama atatoka wa urais visiwani basi makamu toka bara ni mkristo.
Huu ndio uwezekano kwa majina: Kikwete Nje Kwa mantiki ya uislamu. Siyo rais wala makamu. Salim A. Salim ana nafasi kwa mantiki hii ya dini. Nikuchefue zaidi Sumaye na Malecela wanaweza kuwa na nafasi katika mantiki hii. Nimefikiria haya mahesabu usiku nikaona nikushirikishe unipe maoni yako kwa mantiki hii finyu ya udini.

0 Maoni Yako:

Post a Comment

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com