6/19/2005

HUYU NI MMOJA WA WAJUMBE WA TUME YA "AFRIKA"

Mmoja wa wajumbe wa ile Tume ya Afrika ambayo mkuu na mwanzilishi wake ni Waziri Mkuu wa Uingereza, Tony Blair, (sijui Blair alizaliwa kijiji gani Afrika hadi aanzishe tume ya Afrika), ni Waziri Mkuu wa Ethiopia, Meles Zenawi. Kama tuna mtu kama Zenawi kwenye tume ya kujenga Afrika mpya, hiyo Afrika itakuwa na mito ya damu? Fuata viungo hivi usome unyama wa majeshi ya mjumbe huyu wa tume ya "kuiokoa" Afrika. Kongoli hapa, hapa, na hapa.

2 Maoni Yako:

At 6/20/2005 03:49:00 PM, Anonymous Anonymous said...

Kwani hata Mkapa si yuko kwenbye tume? Kuna tofauti gani kati ya serikali ya Tanzania inavyochukulia upinzania na serikali ya Ethiopia? Hii tume ya Afrika inaundwa na wale wale walioiweka Afrika kweny shimo. Tutafika?

 
At 6/21/2005 02:18:00 PM, Anonymous Anonymous said...

Wote wezi tu hao.

 

Post a Comment

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com