6/16/2005

WANAMUZIKI WA AFRIKA KUTUMBUIZA KUPINGA UBEBERU

Mapema leo nilipoandika kwa kirefu na kuweka viungo mbalimbali kuhusu yanayofanyika na yatakayofanyika katika kuelekea mkutano wa nchi 8 kibeberu duniani, nilisema kuwa watu wengi hawaelewi kwanini tamasha la muziki la Live 8, ambalo nia yake ni kutetea Afrika linafanyika bila wanamuziki wa Afrika kushirikishwa. Sasa waandaaji wamegutuka. Wametangaza kuwa wanamuziki wa Afrika watatumbuiza siku ya tamasha hilo, ila katika ukumbi wao wenywe (!!!). Kati ya wanamuziki watakaoshiriki ni mwanamama toka Somalia. Maryam Mursal. Mursal aliwahi kupigwa marufuku kuimba nchini kwake Somalia baada ya kuisakama serikali. Hiyo ilikuwa ni kabla hajakimbilia Ulaya. Baada ya kuzuiwa kuimba alijipatia riziki kwa kuendesha teksi. Hii hapa ni historia yake fupi. Sikiliza mahojiano yake na redio ya NPR. Pia watakuwemo Angelique Kidjo wa Benin na Yossouf Ndour wa Senegal. Habari ya kuwepo kwa tamasha hilo la wanamuziki wa Afrika katika jiji la London iko hapa.

1 Maoni Yako:

At 6/17/2005 03:17:00 AM, Anonymous Anonymous said...

Leaving all the brouhaha about L8 aside, nimefurahi kusikia Maryam Mursal atakuwa mmoja wapo wa wanamuziki hawa. Ndour na Kidjo wanajulikana zaidi lakini Maryam hajapata the recognition she truly deserves.

 

Post a Comment

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com