7/11/2005

Mahojiano BBC Kiswahili na BBC Network Africa

Ndio tumerudi mtaa wa Simba Mweupe, zilipo ofisi za Panos. Tayari tumemaliza mahojiano na kipindi cha BBC cha Go Digital. Nilikuwa na John Kamau. Pia tumefanya mahojiano mafupi kuhusu masuala ya Afrika na mkutano wa wakuu wa makuhani wa ubepari, yaani G8, na Mariam Omar wa idhaa ya Kiswahili ya BBC. Na kesho alfajiri saa kumi na moja na nusu (au ni kumi na moja kamili?...nitahakikisha) nitazungumzia masuala ya uandishi, blogu, na G8 katika kipindi cha BBC Network Africa. Kisha baada ya hapo nitaelekea uwanja wa ndege...chai sijui nitakunywa wapi. Mimi bila chai akili itaacha kufanya kazi! Kamau yeye ataongea na BBC Focus on Africa saa mbili asubuhi.

4 Maoni Yako:

At 7/12/2005 09:29:00 PM, Anonymous Anonymous said...

niliwasikia jana kwenye Go digital , nilifurahishwa na vile huyo jamaa alishindwa kutamka Nde na badala yale akawa anasema N ,De - kana kwamba ni maneno mawili tofauti ... hivyo hivyo hongera kwa kazi njema uliofanya ya kutupasha habari kutoka huko na zaidi kwa kuweza kumshawishi Kamau kuanzisha blogu sasa wacha tusiburi tuone vile atawashikisha wenzake ugonjwa huu wa kublogu kama vile anasema atafanya

 
At 7/13/2005 01:07:00 AM, Blogger Martha Mtangoo said...

Hongera sana Kakaangu wa Damu, nilikupata nikahisi kama nakuona Vile si unajua tena kublog ni kama kaugonjwa flani hivi kaza Buti kwa kuwaelimisha wengine kuwa kama wewe siku moja.

 
At 7/13/2005 02:56:00 AM, Anonymous Anonymous said...

saidi ali na oscar munishi
kaka yetu tulikusikia vizuri sana,unatuwakilisha vizuri sisi,tunakupa go ahead

 
At 7/16/2005 05:30:00 AM, Blogger Reggy's said...

Bahati mbaya sikuweza kusikiliza kipindi chako, lakini naona wanavyokifagilia wanablogu wenzangu, najisikia nilikosa mengi. Nasikitika. Sijui nawezaje kupata walau theme ya yaliyozungumzwa. Nisaidie Bro. -RSM-

 

Post a Comment

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com