8/25/2005

Masahibu ya wanaoblogu kwa lugha zaidi ya moja

Mwanablogu Ethan anajadili kwenye blogu yake masuala ya blogu na lugha. Anagusia blogu zisizo za kiingereza kama blogu za Kiswahili na changamoto waliyonayo wanablogu wanaotumia lugha zaidi ya moja kama Msangi. Ethan msome hapa. Mwanzoni mwa mjadala huu anaongelea mambo ambayo yanaweza yasikuvutie, endelea tu hadi katikati na kisha umalize.

4 Maoni Yako:

At 8/26/2005 06:59:00 AM, Blogger mwandani said...

Tunaandika ili tusomwe. Kimantiki tunataka tusomwe na watu wengi zaidi. Tukiandika kwa kiswahili pekee walengwa wetu ni wanaosema kiswahili, waafrika mashariki pengine kwenye masuala yanayowagusa. Wazo zuri kuandika kwa kingereza na kupanda chati kwenye vyombo vya kuhesabu wasomaji. Je si kweli kwamba walengwa watabadilika kidogo, pengine na mandhari pia?.
Kwa Mfano DJ akipiga muziki kwa ajili ya waafrika wa Afrika mashariki kwenye majumba ya dansi atawapigia vyengine kidogo na vile akienda kuwapigia muziki wapenzi mchanganyiko wa "world music" kwenye matamasha huko ughaibuni... Something's gotta give...

 
At 8/26/2005 07:20:00 AM, Blogger Ndesanjo Macha said...

Mwandani, nakubaliana nawe, hasa unaposema kuwa unapohamia kwenye kiingereza "walengwa na mandhari yanabadilika." Nadhani hata mada zinaweza kuwa tofauti pia. Lakini ni sawa unaposema kuwa umuhimu wa kusomwa na wengi zaidi upo. Nakubali kuwa kiingereza kwa sasa ndio lugha muafaka kwa ajili ya majadiliano ya kidunia. Wakati huo huo hatuwezi kukataa ukweli kuwa majadiliano ya kidunia yanakuwa yameshamiri zaidi yanapoanza miongoni mwa watu wanaoelewana kilugha, kitamaduni, kijiografia, n.k. Na pia wakati mwingine kuna majadiliano ambayo hayahitaji kushirikisha dunia nzima kwahiyo hapo kunakuwa hakuna haja ya kutumia lugha ya kigeni. Nadhani changamoto ndio hiyo anayosema Ethan. Ni vipi mwanablogu wa zaidi ya lugha moja anaweza kufanya kazi yake kwa ufanisi? Kwa ufupi, hoja pande zote zina ukweli fulani.

 
At 8/26/2005 07:36:00 AM, Blogger mwandani said...

Ndugu, masaa yanatafautiana, hivi nimeandika hata sijamaliza kusoma ushajibu? Asubuhi huko kwenu. Haya, Changamoto nzuri, moja ya masuala haya ya mtandao ni ujenzi wa jumuiya kadhaa, za wanaosema kiswahili, wakenya, wapenda miziki, watu wa vyuo kadhaa, wachimbi au ma-"nerd" wa mavyuoni nk. Basi hata tukiandika katika mitazamo ya kiafrika kwa kiingerreza tutakuwa katika jumuiya mojawapo ya watu wenye mitazamo hiyo - tukisomwa pia na wapita njia ambao pengine wanaweza wakawa wasomaji wa kudumu mbeleni. Hapana shaka kama unavyosema, inategemeana na lengo. Ikibidi umombo na umombo utumike. Lengo kusikia msondo, na kuna njia zaidi ya moja ya kuwamba ngoma.

 
At 8/26/2005 08:47:00 AM, Blogger Ndesanjo Macha said...

Mchango poa kabisa. Nakubaliana nawe na nitajazia hoja zako.

Imebidi nicheke kidogo. Kweli lengo ni msondo, kibisa, ukae, n.k. Na sio tu njia ya kuwamba ngoma ni zaidi ya moja bali pia hata namna ya kuzipiga inatofautiana. Kuna wanaopiga kwa mkono, wengine vijiti...ninyi kwenu sijui mnapigaje. Kuhusu kujenga jumuiya mbalimbali (tena na sio wale wanaozungumza kiswahili tu bali, kwa mfano, ndugu zetu Waafrika wa nchi nyingine wasiojua Kiswahili ila wanajua kiingereza...suala hili nikilitazama katika miwani ya kitu wezi wa Afrika walichoanzisha wanachoita umoja wa afrika naona umuhimu wake. Umoja huu lazima watu wa kawaida tuwe na usemi juu yake. Kuna kosa la kufanya umoja huu, kama ule wa Afrika Mashariki kuwa ni muungano wa viongozi wa juu wanaokutana na suti zao na kuweka sahihi na sio muungano wa wananchi unaonzia chini kwenda juu. Ninachotaka kusema kwa kiswahili kifupi ni kuwa waafrika, kwa mfano, tuna mengi ya kujadili sisi kwa sisi ambapo mjadala huo, kwa sasa, hauwezekani bila kutumia lugha za kuazima (kutokana na sababu ambazo wote tunazijua).

Huku ni asubuhi mjomba.

 

Post a Comment

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com