10/14/2005

Ndio Naondoka hivyo

Nitakapoweka kituo katika ukurasa huu nitanyanyua begi la mgongoni, huyoooo...kuelekea kwenye Maandamano ya Mamilioni na Ushee. Nawahi ili nikake viti vya mbele! Nikirudi nataka tuendeleze mjadala alioanzisha Fide. Je ndege ya sirikali inabeba maiti za watoto wa matajiri tu au hata wakeshanjaa? Nitapenda tuanze kujadili jinsi ya kuipiga sirikali marufuku. Kumbuka nitakuwa naripoti mambo yanavyokwenda katika maandamano haya makubwa ya watu weusi.
Baadaye.

2 Maoni Yako:

At 10/15/2005 12:30:00 AM, Blogger mloyi said...

Maandamano ya nini?. Unataka na wewe pia ukifa au ukiumwa ubebwe kwenye ndege ya raisi? Unajua binadamu wote ni sawa na sawasawa pia? Kwani yalianzia kwenye sirikali tu? angalia hata makanisani ukitoa sadaka kubwa unapewa nafasi kubwa pia/ huoni hayo yataendelea mpaka kwa mungu mbinguni tukiwa tunaelea mawinguni kama moshi mweupe wa papa? Kwani wewe unalipa kodi kiasi gani mbona huulizi wao wanalipa kodi kiasi gani na wewe pia uombe kulipa kiasi hichohicho? au ni wivu tu?

 
At 10/16/2005 01:44:00 AM, Anonymous Anonymous said...

Kodi? Mmmgh!? Kodi pale nyumbani analipwa nani? Kodi pale nyumbani inalipwa wapi? Pale Samora Avenue au kule karibu na stesheni? Halfu ikishalipwa inafanyiwa nini? Walevi tuliopata kunywa Stelle Artois tulikuwa hatujui kwamba ile bia iliingizwa na muhindi ambaye alisamehewa kuilipia kodi! Waziri Mbilinyi alifukuzwa kazi kwa sababu ya kusamehe kuwalipisha kodi matajiri kadhaa! Kama ni kodi marehemu bibi yangu kailipa sana kwa kuuzia tena kwa mkopo pamba vyama vya ushirika. Kalipa sana kodi kule Ukerewe kwa mikiki ya wanamgambo na wajumbe wa chama wa kule Ukerewe. Kama unakumbuka polisi, mgambo, na vijana wa chama (TANU Youth League hadi UV-CCM) wamekimbiza sana wananchi kulipa kodi. Msako wa nyumba kwa nyumba umefanywa sana kwa wazawa mijini na vijijini hali kadhalika lakini walikuwa hawabishi hodi nyumba za Wahindi Kisutu kuwauliza mahouse wife na watoto wasio na kazi kama wamelipa kodi!
Wapo Watanzania ambao maisha yao yote (mathalani walimu vijijini)wanalifanyia kazi taifa katika mazingira magumu na wanalipa kodi kutoka katika mishahara inayocheleweshwa hata kwa miezi. Watu hawa hata wakifa huko walipoajiriwa maiti zao zinasafirishwa kwa pesa za maskini wenzao, ndugu, jamaa, na marafiki. Hakuna fungu serikalini la kusafirisha maiti za waaajiriwa wa serikali toka sehemu walizoajiriwa mpaka makwao kwa asili! Marehemu Charles Zawosse alikuwa achomwe moto na Halmshauri ya jiji la Stockholm kwa sababu ya kukosa pesa za kumsafirisha kurudi nyumbani. Ubalozi wa Tanzania Stockholm ulidindisha katakata kwamba hakuna fungu la kusafirishia maiti za Watanzania. Asante nyingi ziwaendee Bwana John Simson wa Real Records na Bi Jaana-Maria Jukkara wa Global Music Center, Helsinki kwa kuchukua jukumu la kumsafirisha Marehemu Charles kwa pesa zao wenyewe.
Kama sera ya uwazi na ukweli ni sera ya kweli waturuhusu kuangalia utajiri wa hao matajiri kama ni utajiri wa haki au dhuluma. Kama hao matajiri wana madeni na benki ya zamani NBC au CRDB au benki yoyote iliyokuwa ya serikali na kama wamelipa hayo madeni yao. Ninakuambia tena kwa uhakika tutawakuta na madeni ambayo hayajalipwa na hayajulikani kama yatalipwa.
Mungu Ibariki Tanzania,
Fidelis MtiMkubwa Tungaraza, Helsinki, Finland.

 

Post a Comment

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com