1/09/2006

Jarida Pepe la MBONGO

Unakaribishwa kwa mikono miwili na bilauri ya maji na ndugu yetu Semkae Kilonzo. Anakukaribisha kwenye tovuti ya habari iitwayo Mbongo (ambapo utakutana na kona ya Michuzi). Kilonzo kaniambia jambo moja la msingi sana. Anasema kuwa ni jambo la busara iwapo tutaunganisha nguvu za blogu na tovuti katika kujenga jamii mpya. Nadhani swali moja ambalo ndugu yetu hawaweza kuliepuka toka kwetu ni lugha inayotumika kwenye tovuti ya Mbongo. Kilonzo, mbona?
Bonyeza hapa utembelee tovuti hiyo.

6 Maoni Yako:

At 1/10/2006 05:12:00 AM, Blogger FOSEWERD Initiatives said...

kaka ndesanjo, nimetembelea jarida hilo na ni zuri. ni jamnbo la msingi kabisa nakubaliana katika kujenga jamii mpya. nilicheka sana siku moja nilitembelea tovuti ya wakenya wanaseam kuwa unashuka na ndege nairobi halafu unaenda kilimanjaro kupanda mlima. walichosema ni kuwa arusha airport isiwe confused na arusha karibu na kilimanjaro.

hili suala la lugha labda ni la kuangalia vizuri. maana yangu kuangalia walengwa. kukwepa kingereza wakati unaitangaza nchi ni ngumu. maana walengwa wako huko nje, na pengine hawajui kiswahili. labda kwa manufaa ya watalii wa ndani na wale wa kujifunza kiswahili jarida liwe na options za lugha - kama kiingereza au kiswahili (lugha mama). pia baadae hata kifaransa na kijerumani. ndio tanzania mpya!

 
At 1/12/2006 12:15:00 PM, Anonymous Anonymous said...

Mark,

Ni kweli kabisa tatizo letu sisi ambao tunategemewa huku tufanye kazi ya kibalozi ya kuiwakilisha nchi yetu ni muhimu kutoweka lugha hii ya kiingereza mbali nasi.

Ni kweli ile portal ya http://www.mbongo.com ni ya kiingereza ila tujaribu kuwa kwa lugha ya kigeni, 'bi-lingual'. Jambo ambalo hawa wenzetu huku wanachotuonea donge ni uwezo wetu wa kuongea lugha 2 au tatu bila tatizo. Sasa naombeni wanablogu na wanatovuti tuungane kwa nia moja ya kukuza utamaduni wetu duniani.

Halikadhalika, naombeni mtembelee Pare katika ensaiklopidia ya wikipedia muone navyojaribu kuweka watu wa bush kwetu kwenye ramani. Nilihamasishwa baada ya kuona watani zetu wachaga wamejipamba kweli kweli. Sasa na nyie watu wa kabila zingine tuwakilisheni.

Tanzania tusipojitanganza nani atatufanyia hiyo kazi?

 
At 1/15/2006 08:17:00 AM, Blogger Ndesanjo Macha said...

Mark na Semkae,
Mimi sina tatizo lolote na Kiingereza. Kwanza ninayo blogu ya Kiingereza (sio hii ya Kiswahili tu). Kila mara huwa nasema kuwa lugha ina kazi kuu mbili: 1. chombo cha mawasiliano 2. benki ya maarifa. Lugha huhifadhi maarifa na elimu kupitia nyimbo, fasihi simulizi/andishi, misemo, methali, hekaya, n.k.

Kiingereza nakitumia kwa kazi namba moja (chombo cha mawasiliano) kwa ajili ya kuwasiliana na wale ambao hawajui lugha nyingine ninazojua ila wanajua kiingereza. Hapo sina tatizo. Ila ninapokuwa ninawasiliana na wale ambao wanafahamu lugha za Kiafrika ninazoongea, sina sababu ya kuazima lugha toka Uropa. Na pia ninapokuwa katika jitihada za kulinda utamaduni wangu na kuhifadhia maarifa yangu ya asili, ya watu wangu, natumia lugha yangu.

Nakubaliana kuwa kama unataka watu nje ya Tanzania kujua juu ya nchi yetu, basi utatumia kiingereza. Lakini pia unaweza kutumia kiswahili maana watu wa Kongo, Rwanda, Oman, visiwa vya Komoro na Shelisheli,n.k. wanaongea Kiswahili na wao pia ni vyema wakajua kuhusu Tanzania. Jambo la msingi ambalo siwezi kupinga ni kuwa inategemea hadhira yako ni akina nani.

Tovuti ya Mbongo ambavyo ilivyo sasa (ukitazama majadiliano ya wasomaji, habari zake, n.k. na pia msemo "where Tanzanians click" inaonekana kuwa hadhira yake kwa kiasi kikubwa ni Watanzania. Ninaweza kusahihishwa kama nimekosea. Ila nimetembelea sehemu ya majadiliano kuona wanaoshiriki ni akina nani na mambo wanayoongelea ni mambo gani nikakuta ni kaka na dada zangu wa Tanzania. Nikaangalia habari za ukurasa wa mbele nikakuta habari zilizoko zinaelekea kuwa zimelengwa kwa Watanzania na ni za matukio ya kila siku na sio habari za kutangaza nchi kwa watu tunaowaita watalii. Sisemi kuwa kuna ubaya kuwa na habari kama hizo. Nadhani juhudi kama hizi, za kuanzisha tovuti, ni muhimu sana katika zama hizi ambazo sehemu kubwa ya uchumi na nyanja ya maendeleo zitakuwa zikiendeshwa na zana mpya za mawasiliano na habari.

Suala la kuitangaza Tanzania ili "watalii" wakaitembelee nitalizungumzia baadaye kwenye ukurasa wa mbele wa blogu yangu maana nadhani tunafanya kosa sana tunapohusisha wazungumzaji wa kiingereza na utalii. Tunapotaka watu wanaoishi maili maelfu kwenda kutembelea sehemu mbalimbali za kihistoria nchini kwetu huku tukiwa hatuhamasishi watu wetu kutembelea sehemu hizo. Kabla sijamtangazia mzungu kuwa kuna michoro kwenye mapango kule Dodoma au Singida, nitataka kwanza wakazi wa maeneo hayo wajue kuwa kuna michoro hiyo. Ningependa watoto wa shule maeneo hayo wajue kuhusu michoro hiyo, historia yake na nafasi yake katika utamaduni wetu.

 
At 1/15/2006 08:25:00 AM, Blogger Ndesanjo Macha said...

Semkae,
Usisahau kuwa nasi tunajenga kamusi elezo ya wiki ya Kiswahili (wikipedia ya kiswahili). Hivi sasa tuna makala 180. Iko hapa:
sw.wikipedia.org

 
At 1/15/2006 02:35:00 PM, Anonymous Anonymous said...

Safi sana hiyo wiki ya kiswahili. Mnafanya kazi nzuri sana. I will join soon.

 
At 1/17/2006 04:35:00 AM, Anonymous Anonymous said...

Kupata watalii ni jambo bora/muhimu na si la lazima kama vile kupata hewa na chakula. Lugha ikiwemo Kiswahili, ina maana kubwa sana katika jamii yetu. Lakini toka enzi za kuchanganyika na wageni tumeona vitu vyetu na hata lugha yetu ni duni. Kuna mataifa mengi duniani yameendelea wakati si watumiaje wa kiingereza. Sisi pia tumo kwenye kundi hili na maendeleo yetu si lazima yategemee kiingereza.

 

Post a Comment

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com